Categories: Education

Usiku utakapokwisha

  • ISBN: 9789987871919
  • Product format: Paperback
  • Author: Mbunda Msokile
  • Publisher: APE Network
  • Year published: 2021
  • Availability: In stock
7,000 TZS

Product description

Mbunda Msokile alizaliwa Mbinga, Tanzania. Alipata elimu ya msingi katika shule za Wukiro na Litembo, na elimu ya sekondari katika shule za Kigonsera na Ihungo. Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu shahada ya B.A (Ed)

Qty

Tab Article

Mbunda Msokile alizaliwa Mbinga, Tanzania. Alipata elimu ya msingi katika shule za Wukiro na Litembo, na elimu ya sekondari katika shule za Kigonsera na Ihungo. Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu shahada ya B.A (Ed) mwaka 1976. Mbunda alifanya kazi ya ualimu katika shule mbalimbali za sekondari kabla ya kurudi tena Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1979 kama mhariri kwenye kitengo cha Dar es Salaam University Press (DUP).
Mbunda ameandika vitabu mbalimbali, vikiwamo: Misingi ya uhakiki wa Kiswahili, Misingi ya hadithi fupi, Historia ya matumizi ya Kiswahili na Kunga za fasihi na lugha.
Usiku utakapokwisha ni riwaya inayochambua na kubainisha matatizo yanayoikumba jamii, hususani yale ya kiuchumi, kama vile ukosefu wa ajira. Matatizo haya yanawafanya vijana watatu, Chioko, Gonza na Nelli washindwe kufikia ndoto za maisha yao. Kila wakitamani kupata furaha na tulizo la moyo,
shauku yao inagonga mwamba wa dhiki za maisha! Hivyo wanajikuta katika balaa … ndipo tunaposikia kilio cha uchungu cha Gonza akisema, “Kwa nini kabwela tulambe kamasi na wengine asali?” Aidha sauti ya huruma na ushauri ya rafiki yake, Chioko, inasema, “… shida hizi tunazo siku zote. Leo hii hasira
zinakujaje?”
Gonza hakubaliani na hilo. Anaamua kutumia njia ya mkato kushinda dhiki za maisha. Hata hivyo, ndoto na harakati zake zinakatika ghaa ... Yanabaki masikitiko ya Chioko, “Gonza … umemtekenya punda miguu yake ya nyuma, ukapata shukurani zake. Ulitakiwa uwe na subira na utulivu hadi pambazuko ...” Je, nini kilizima harakati za Gonza? Je, usiku utakwisha lini?

0 reviews for Usiku utakapokwisha

Add a review

Your Rating