Categories: Self-help

Siri ya Binadamu Kuishi Miaka Mingi - Nguzo 72 Zinazoshikilia Uhai Wako

15,000 TZS

Product description

Ndugu Pius Bakengera Ngeze (pichani), katika kitabu hiki, Siri ya Binadamu Kuishi Miaka Mingi: Nguzo 72 Zinazoshikilia Uhai Wako, ametumia uzoefu wa umri wake, uandishi na usomaji wa vitabu na machapisho mengine kuwaandikia Wosia binadamu kuhusu jins

Qty

Tab Article

Ndugu Pius Bakengera Ngeze (pichani), katika kitabu hiki, Siri ya Binadamu Kuishi Miaka Mingi: Nguzo 72 Zinazoshikilia Uhai Wako, ametumia uzoefu wa umri wake, uandishi na usomaji wa vitabu na machapisho mengine kuwaandikia Wosia binadamu kuhusu jinsi ya kuishi miaka 80-100. Kitabu hiki kimezingatia mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Matibabu na uelewa uliopo duniani kuhusu elimu mpya ya kumwezesha binadamu kuishi miaka mingi.

Ni kitabu cha aina yake ambacho kila mwanadamu anayependa kuishi miaka mingi anapaswa kukimiliki, kukisoma na kukirejea mara kwa mara.

Siri ya Binadamu Kuishi Miaka Mingi iko ndani ya kitabu hiki. Kwa hiyo, ni muhimu ukisome ili uweze kuigundua. Uhai ulionao leo ni zawadi kuu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Jukumu lako ni kufanya uamuzi wa kuutunza (uhai huo) kwa kipindi kirefu kadiri inavyowezekana au kwa kipindi kifupi. Si jukumu lake, ni jukumu lako. Ukipewa zawadi na mtu anayekuthamini au anayekupenda, ni jukumu lako kuitunza vizuri ili iweze kukufaa kwa kipindi kirefu au kutoitunza na matokeo yake utaifaidi kwa kipindi kifupi. Hali ndivyo ilivyo kwa zawadi ya uhai tuliyopewa na Mungu.

Kila mtu anapenda kuishi miaka mingi na iwe ya furaha, isiwe ya dhiki, shida na afya mbaya kwa kipindi kirefu. Lakini, hayo ni matarajio na matumaini tu.

Pamoja na kujitahidi kutekeleza Nguzo hizo, endelea Kumtegemea na Kumwomba msaada Mungu. Bila yeye huwezi kitu. Kwake hakuna lisilowezekana.

0 reviews for Siri ya Binadamu Kuishi Miaka Mingi - Nguzo 72 Zinazoshikilia Uhai Wako

Add a review

Your Rating